Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema watendaji ambao maeneo yao
yataendelea kukithiri kwa vitendo vya uhalifu, migogoro ya ardhi,
uharibifu wa mazingira na uchafu atawatumbua majipu.
Akijibu
swali aliloulizwa na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu
kuibuka kwa vitendo vya uvamizi, uporaji na mauaji katika jiji la
Mwanza, alisema Serikali haitavumilia kuona watu wasio na hatia
wakipoteza maisha na mali zao huku wenye dhamana ya ulinzi wakikaa bila
kuchukua hatua.
Mongella alisema: “Sitasubiri nitumbuliwe mimi, nitawatumbua kwanza viongozi na watendaji wazembe kabla sijatumbuliwa.
“Kwa
kipindi cha wiki mbili nilichokaa Mwanza kumetokea matukio mawili ya
wafanyabiashara ya maduka ya fedha kwa njia ya mtandao kuvamiwa, kuporwa
na wengine kuuawa kwa kupigwa risasi, hii haikubaliki na siko tayari
kushuhudia vifo vingine."
Post a Comment