Diamond Platnumz amemaliza ziara yake ya Ulaya aliyoipa jina, From
Tandale to The World Tour iliyompeleka kwenye nchi takriban nane.
Show yake ya mwisho ilifanyika Jumamosi hii jijini Copenhagen, Denmark ambayo video zake inaonesha ilikuwa na mafanikio makubwa.
Mchumba wake Zari aliyemsindikiza kwenye nchi zote alizopita, ameshukuru
kwa kuandika: Allow me to thank everyone that helped us while out there
in Europe. For showing us around and hosting us. Mostly thank you for
allowing my hubby entertain you. Stay blessed.
Tayari Zari amerejea Afrika Kusini kuungana na familia yake.
Katika hatua nyingine Diamond amedai kuwa reality TV show yake ijayo itaweka wazi mambo mengi mazito.
“Can you try to guess the name of our Reality Show?) (Muda si Mwingi
Kipindi cha Maisha yangu ya kila siku, Familia na Team yangu nzima
itaanza kuwa kwa Tv yako pendwa, ” ameandika Instagram.
“Nakuahidi sio tu eti Kireality show … ni Reality show Bora ambayo
naamini utaipenda kunzia kwenye Quality, Mikasa na matukio yote
nnayopitia mimi, Familia na Team yangu kila siku….Mengi yanaonekana,
Unayoyasikia, Unayasoma ila kwenye Hiki kipindi ndio itakuwa Thibitisho
la kila uvumi uusikiao….Sjui Kipini puani, Mara jicho, Mara sjui
@officialshetta , Mara DNA, Mara @romyjons kutoinekana tena kwenye Tour
Ghafla….Niamini mimi yote utaona na kuyapata kwa uwazi kabisa, Kaa na
Mimi…….! We unavyohisi reality Show yetu itakuwa inaitwaje…..?”
ameongeza.
Monday, 11 April 2016
Diamond Amaliza ziara ya Ulaya, Adai Reality TV Show yake itaweka Wazi Mambo Mazito
Posted by Unknown on 07:56:00 in BURUDANI | Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment