TAMBWE |
Ilikuwa kama utani, lakini sasa ni kweli kwamba Yanga imerejea kileleni baada ya kufikisha pointi 50.
Yanga
imerejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa African Sports ya
Tanga kwa mabao 5-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Ushindi
huo ulikuwa muhimu kwa Yanga baada ya kuwa imeondolewa na Simba
kileleni. Simba walifikisha pointi 48 baada ya kuitwanga Mbeya City kwa
mabao 2-0.
Ubishi ukawa ni Simba itakaa kwa muda mfupi na wenye kilele ni Yanga. Kweli wamerejea baada ya ushindi huo wa mabao 5-0.
Shukurani
kubwa kwa Amissi Tambwe aliyefunga mabao mawili, Kelvin Yondani, Donald
Ngoma na Anthony Simon Matheo ambao walikamilisha idadi hiyo ya “mkono”
ya Yanga.
Mechi
ilikuwa ya ushinda, Sports wakionekana wagumu katika dakika za mwanzo
lakini kadiri muda unavyozidi kusonga mbele, wakazidi kupoteza mwelekeo
na kutoa nafasi kwa Yanga “kufanya yao”.
Post a Comment