Baba Mtakatifu Francisko tarehe 15 Machi 2016 majira ya 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya, anatarajiwa kuongoza kikao cha kawaida cha Makardinali, ambamo Kanisa litapitisha majina ya wenyeheri watano, wanaotarajiwa kutangazwa kuwa watakatifu kwa mwaka mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu. Wenyeheri hawa ni:
- Giuseppe Sànchez del Rio.
- Stanslao di Gesù Maria.
- Giuseppe Gabriele wa Rozari Takatifu.
- Maria Elizabeth Hesselblad
- Mama Theresa wa Calcutta aliyefahamika kama Agnese Gonxha Bojaxhiu.
Post a Comment