March 12 klabu ya Dar Es Salaam Young
African ya Tanzania ilishuka katika uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda
kucheza mchezo wake wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu
Bingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao timu ya jeshi APR ya Rwanda.
Yanga imeaingia kucheza raundi ya pili
ya michuano hii, baada ya kuitoa klabu ya Circle de Joachim ya
Mauritius. Katika mchezo wa raundi ya pili Yanga ilifanikiwa kuitambia
APR ya Rwanda kwa kuifunga jumla ya goli 2-1, licha ya kuwa APR ilikuwa
nyumbani na kupata sapoti kubwa ya mashabiki wanajeshi.
Magoli ya Yanga yalianza kufungwa dakika
ya 21 baada ya Juma Abdul kupiga faulo na kufunga kwa kushuti kali,
hiyo ilikuwa baada ya Donald Ngoma kuchezewa faulo. Thabani Kamusoko
alirudi wavuni dakika ya 75, wakati jitihada za APR ziliishia kuzaa goli
moja tu dakika ya 90 kupitia kwa Patrick Sibomana.
Post a Comment