Mtu tajiri zaidi nchini Brazil amehukumiwa kifungo cha miaka 19 jela kwa kushiriki ufisadi.
Mfanyibiashara
huyo mashuhuri katika sekta ya ujezi, Marcelo Odebrecht, alipatikana
na hatia ya kuhusika katika ufisadi unaohusu viwango vikubwa vya fedha .Mahakama ya huko inasema kuwa Bw. Odebrecht amepatikana na hatia ya ulanguzi wa pesa , utoaji hongo na pia kuwa na ushirikiano na watu wahalifu.
Aidha Mahakama hiyo imesema Odebrecht alilipa hongo ya hadi dolla millioni 30 kwa kampuni kubwa ya mafuta nchini humo Petrobras,ili apendelewe na kupewa kandarasi.
Amekuwa kizuizini tangu mwezi Desemba.
Kampuni yake ya Odebrecht ndio kubwa zaidi katika kanda ya Amerika ya Kusini ambako inahudumu katika mataifa 21.
Vilevile Odebrecht imewaajiri wafanyikazi katika kanda zima katika sekta ya ujenzi.
Bwenyenye huyo alijiuzulu kutoka kwa kampuni hiyo ilioanzishwa na familia yake na ambako amekuwa akifanya kazi.
Post a Comment