Rais
John Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi
karibuni na katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya
kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.
Rais
Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao
watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao
wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.
"Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu.
"Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.
"Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana.
"Haiwezekani vijana leo hii unawakuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli ameongelea pia suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini ambapo amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.
"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll
"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll
"Mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani
"Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202. Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.
"Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani( selo) hata masaa 48,wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa.
"Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani( selo) hata masaa 48,wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa.
"Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele."Amesema Rais Magufuli
Post a Comment