Mother Teresa alikuwa mtawa wa kanisa Katoliki
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametangaza kwamba Mother Teresa atafanywa mtakatifu Septemba mwaka huu.
Sherehe ya kumtawaza kuwa mtakatifu itafanyika tarehe 4 Septemba.
Njia ya
kumfanya mtakatifu ilifunguliwa Desemba mwaka jana baada ya Vatican
kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea
mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake.
Mother
Teresa alipewa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na huduma yake kwa raia
maskini kwenye vitongoji vya jiji la Calcutta nchini India.
Alizaliwa
1910 eneo ambalo kwa sasa hujulikana kama Macedonia na wazazi wa asili
ya Albania na kupewa jina Agnes Gonxha Bojaxhiu.
Alipewa uraia kamili wa India baada ya kuanzisha kikundi cha watawa cha Missionaries of Charity mwaka 1950.
Alifariki 1997 akiwa na umri wa miaka 87. Alifanywa mbarikiwa mwaka 2003.
Post a Comment