BREAKING NEWS

Saturday, 12 March 2016

Ester Bulaya Awasili Jijini Mwanza Baada Ya Kuhojiwa Kwa saa tatu na Kisha Kuachiwa Huru


Mbunge  wa  Bunda  mjini.Ester Bulaya   amewasili  jijini  mwanza  usiku  huu  baada  ya  kuhojiwa  kwa  masaa  matatu  jijini  Dar  na  kikao  cha  kamati  ya  haki, kinga  na  madaraka ya  bunge.

Bulaya  alikamatwa  usiku  wa  manane  wa  kumkia  leo  kwa  amri  ya  spika  wa  bunge  ambapo  alisafirishwa  hadi  jijini  Dar es Salaam   kwa  ndege  kujibu  tuhuma zinazomkabili.

Akiongea  na  waandishi  wa  habari  baada  ya  kurejea  jijini  Mwanza usiku huu, Bulaya  amesema  anashangazwa  na  kitendo  cha  serikali  kutumia  pesa  na  nguvu  nyingi  kumkamata  wakati  pesa  hizo  zingeweza  kutumika  kuboresha  maisha  ya  askari  polisi 

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree