Mwanafunzi
wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi mkoani
Mtwara, Tawfiq Hamisi (17), amefariki dunia baada ya kukatwa na kiwembe
katika mkono wake wa kulia na mwanafunzi mwenzake Issac Yohana (16).
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry
Mwaibambe, amesema kabla ya kifo hicho kulikuwa na ugomvi kati ya
marehemu na mtuhumiwa ambaye ni Isaac anayedaiwa kuficha kiatu cha
mwenzie ambapo baada ya mzozano akaamua kumkata na kiwembe mwenzie chini
ya bega lake la kulia.
Ameongeza
kuwa marehemu ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga huku mtuhumiwa ni mwenyeji
wa wiayani Newala mkoani Mtwara, na kwamba taratibu za kuusafirisha
mwili wa marehemu kuupeleka kwao zinafanywa na uongozi wa shule, huku
mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya Ligula, Dkt. Mdoe Mhuza, amethibitisha
kupokelewa kwa mwili wa marehemu majira ya saa 11 alfajiri na kudai kuwa
bado uchunguzi zaidi unaendelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanzo cha
kifo chake.
Post a Comment