BREAKING NEWS

Wednesday, 3 February 2016

Ushindi wa Simba dhidi ya Mgambo JKT umeisaidia kuisogelea Yanga kileleni, Matokeo ya mechi za VPL Feb 3





Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo February 3 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti tofauti Tanzania, klabu ya Dar Es Salaam Young Africans ilikuwa mgeni wa klabu ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati watani zao wa jadi Simba walikuwa wenyeji wa Mgambo JKT uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

DSC_0597 

Simba ambao kwa sasa wapo na kocha wao msaidizi Jackson Mayanja bila kuwa na kocha mkuu wamefanikiwa kuendeleza hali ya ushindi kwa kila mechi, baada ya mchezo wao wa wiki iliyopita dhidi ya Africans Sports kuibuka na ushindi wa goli 4-0. February 3 Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi mwingine mnono dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa Taifa, kwa kuwafunga idadi ya goli 5-1.

DSC_0589 

Wekundu wa Msimbazi Simba walikuwa mahiri katika kuuchezea mpira, kwani dakika ya 5 tu walifanikiwa kupachika goli la kwanza kupitia kwa Hamis Kiiza, kabla ya Mwinyi Kazimoto hajafunga goli la pili dakika ya 28 na Ibrahim Ajib kufunga goli la tatu dakika ya 45. Kipindi cha pili Simba waliendeleza ubabe baada ya dakika ya 77 Danny Lyanga kupachika goli la nne.

DSC_0620 

Mshambuliaji wao tegemeo Hamis Kiiza alihitimisha ushindi huo kwa kufunga goli la tano, Mgambo walipata goli la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Fully Maganga baada ya ngome ya ulinzi ya Simba kujisahau. Kwa matokeo hayo Simba wanakuwa nafasi ya pili wakiwa na point 39 nyuma ya Yanga kwa tofauti ya point moja.

DSC_0586 

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa February 3
  • Prisons 2 – 2 Yanga
  • Kagera Sugar 2 – 1 Majimaji FC
  • Africans Sports 1 – 0 Mwadui FC
  • Mtibwa Sugar 2 – 2 Toto Africans


 

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree