Umoja wa mataifa umeahirisha
mazungumzo ya amani yaliyolenga kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
nchini Syria yaliyodumu kwa miaka mitano.
Mjumbe maalum wa umoja
wa mataifa anayeshughulikia mgogoro huo,Staffan de Mistura amesisitiza
kuwa mazungumzo hayo hayajashindikana na yatafanyika tena tarehe 25
mwezi Februari.Pande zote mbili zimelaumiana kusababisha kusitishwa kwa mazungumzo hayo.
Hatua hii imekuja wakati Serikali ya Syria ikisema imevunja ngome ua upinzani mjini Aleppo.
De Mistura amekiri kuwa jitihada zaidi inapaswa kufanyika
Kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Syria Bashar Jafaar ameshutumu upinzani kusukumwa kwa nguvu ya Saudi Arabia, Qatar na Uturuki na kuchangia kushindikana kwa mazungumzo, televisheni ya taifa nchini Syria imeripoti.
Upinzani nao umeilaumu Serikali na kusema kuwa hawatarejea kwenye mazungumzo mpaka hali itakapoimarika Syria.
Upinzani umeghadhabishwa na kitendo cha vikosi vya serikali ya nchi hiyo kuendelea na mashambulizi mjini Aleppo wakati mazungumzo yakiendelea
Post a Comment