WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameitaka Bodi mpya
ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia upya mkataba wa
StarTimes na shirika hilo.
Amesema
kumekuwa na maneno kuhusu mkataba huo, hivyo bodi inapaswa kubainisha
vifungu vya sheria ambavyo vitahitaji kufanyiwa marekebisho.
Akizungumza
katika uzinduzi wa bodi mpya chini ya Mwenyekiti wake, Balozi Herbert
Mrango, Nape alisema mapitio hayo yanaweza kufanyika ndani ya mwezi
mmoja, kubaini mapungufu yaliyopo.
“Bodi
hii inapokea majukumu yaliyoachwa na bodi iliyopita. Majukumu hayo ni
pamoja na kupitia upya mkataba wa StarTimes na TBC kwani mkataba uliopo
utaisha na utatakiwa kuwa na mkataba mpya,’’ alisema Nape.
Pia
aliitaka bodi hiyo kuhakikisha kwamba baada ya miaka minne, TBC
inajiendesha yenyewe kiuchumi kwa kuzingatia uwekezaji katika viwanja
vyao.
Alisisitiza
kuwa ni vyema bodi hiyo ikaangalia upya muundo wa shirika hilo na
kwamba wawashirikishe wafanyakazi ili wajue nafasi zao.
Post a Comment