
MWENYEKITI
CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amewaomba wazee kote nchini, kumuunga
mkono Rais John Magufuli katika uongozi wake ili kumpa moyo wa
kuwatumikia Watanzania.
Amesema
kipindi ambacho Dk Magufuli ameingia madarakani hadi sasa ni muda
mfupi, hivyo si vema kuanza kudodosa na kulaumu panapopwaya, badala yake
Wazee na watanzania kwa jumla wazidi kumuunga mkono ili kumtia moyo wa
kutekeleza yote aliyokusudia kuyafanya kwa manufaa ya taifa.
Kikwete
alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa
wa Singida, ambapo alisema kuwa kuongoza bila ushauri wa wazee nchi
inaweza kuyumba.
“Kuongoza
nchi bila wazee mambo hayaendi vizuri na ukikosa mzee kwenye jahazi
wapiga makasia vijana wanaweza kuanza kuzozana na chombo kwenda mrama,
lakini wakiwepo wazee watawaongoza vizuri na chombo/ nchi kwenda
salama”. Alisema Kikwete huku akishangiliwa na wazee.
Alisisitiza
kwamba ukitaka nchi itulie kamata wazee, lakini ukiongoza nchi kwa
kutumia vijana pekee nchi inaweza kuyumba, na itafika mahali mtakosa
mahali pa kushika.
Alisema
kuwa hata yeye kwa mara ya kwanza .alipokwenda kuomba ubunge jimboni
kwake Bagamoyo, Pwani aliunda kamati ya wazee ambayo ilimsaidia sana.
Wazee ni sehemu ya matumaini ya chama na Serikali, panapokuwepo wazee hapaharibiki jambo.
“Nawashukuru sana wazee endeleeni kukijenga chama na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa sasa na Dk John Magufuli.” Alisisitiza Kikwete na kuongeza kuwa,
“Hata
kwenye chama chetu tumeunda Baraza la Washauri la Wazee wasitaafu
ambapo wengi walipinga. Hata hao wazee tuliowataka waunde baadhi yao
walipinga, lakini mwisho walikubali kwa masharti kwamba wawe wanaitwa
panapotokea jambo kubwa litakalohitaji ushauri wao.”
Alisema
mmoja wa viongozi aliyekuwa msitari wa mbele kuunda baraza hilo alikuwa
Rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alitoa ushauri wa
kuitwa kutoa ushauri panapotokea jambo kubwa na kwamba hata wakitoa
ushauri, viongozi waliopo madarakani wawe hiari kuukubali au kuukataa.
Aliwataka
wazee kuendelea kuiunga mkono serikali ya sasa ambayo kwa hivi sasa
imetimiza muda mfupi wa miezi mitatu ambaye ni sawa na mtoto mdogo
anayekua.
Alisema
kuwa Jambo kubwa ni kuwaunga mkono, kuliko kuwalaumu ama sivyo
watavunjika moyo, ndani ya miaka mitano itakuwa hasara. ...."Watieni moyo ili wajiamini wahudumie vizuri zaidi ili nchi isonge mbele kimaendeleo."
Kikwete
alisisitiza kuwa hata yeye akitakiwa kwenda kutoa ushauri atakwenda na
akiwa na jambo la kushauri atakwenda pia, lakini aliwaasa kuwa si kila
jambo wazee watake kwenda kutoa ushauri, itachelewesha mambo mengi.
Post a Comment