
Kambi
rasmi ya upinzani bungeni, imetangaza baraza lake la mawaziri kivuli
ambalo Chama cha ACT Wazalendo, chenye mbunge mmoja, Kabwe Zitto, ndicho
hakikuingizwa kwenye baraza hilo. Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe
alitangaza jana bungeni baraza hilo.
Chadema
chenye wabunge wengi katika kambi hiyo, kina mawaziri vivuli wengi
ikilinganishwa na vyama vingine na wakati huo huo, kina wizara nyingi
ambazo kinaongoza peke yake kwa maana ya kuwa na mawaziri na naibu
mawaziri vivuli.
Mbowe alisema idadi ya wizara alizotangaza inafanana na ya wizara za Serikali ya Awamu ya Tano ambazo zipo 19.
Mbali na kutangazwa kwa majina hayo ,Bunge lilifanya uchaguzi wa wajumbe wa kuliwakilisha kwenye taasisi mbalimbali za kibunge.
Wajumbe
hao ni wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Bunge la Afrika (PAP), Jukwaa la
Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF), Kamati ya
Utendaji wa Bunge la Jumuiya ya Madola (CPA) na Umoja wa Wabunge Duniani
(IPU).
Akitangaza
wabunge walioshinda katika uchaguzi huo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas
Kashililah alisema idadi ya wajumbe waliorudisha fomu za kuwania nafasi
hizo ilikuwa inalingana na idadi ya nafasi zilizokuwa zikiwaniwa, hivyo
kuwafanya wote kupita bila kupigiwa kura.
1.Tume ya Utumishi wa Bunge Kangi Lugola, Fakharia Shomar Khamis, Mary Chatanda, Mussa Azzan Zungu, Salim Hassan Turky, Magdalena Sakaya na Peter Msigwa.
2.Bunge la Afrika Mboni Mhita, Asha Abdullah Juma, Dk Faustine Ndugulile, Stephen Masele na David Silinde.
3.Jukwaa la Wabunge wa SADC Jamal Kassim Ali, Esther Mmasi, Selemani Zedi na Ally Abdallah Saleh.
4.Kamati ya Utendaji ya Bunge la Jumuiya ya Madola
Amina Mollel, Maria Kangoye, Zainab Vullu, Khamis Mtumwa Ali, Salum
Rehani, Japhet Hasunga, Josephat Kandege, Dk Raphael Chegeni, Jitu Soni,
Immaculate Semesi, Juma Hamad Omar na Tundu Lissu.
5.Umoja wa Mabunge Duniani Dk Pudenciana Kikwembe, Juma Othman Hija, Mohamed Mchengwerwa, Peter Serukamba na Susan Lyimo.
Post a Comment