Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho ameingia kwenye headlines baada ya refa kumuomba Ronaldinho asaini
kadi yake ya njano kama ambavyo wengi huwa wanafanya wanapokutana na
mastaa huwa wanaomba kusainiwa vitabu vyao vya kumbukumbu na watu
maarufu.
Katika maisha hutokea mara chache sana mtu kupata bahati ya kukutana na staa wa kiwango cha dunia, Ronaldinho ambaye alikuwa Ecuador
kucheza mchezo wa hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha, aliingia
kwenye headlines baada ya mapumziko refa kuomba apate saini ya Ronaldinho lakini kwa sababu hakuwa na kitabu cha kumbukumbu ikabidi kuomba Ronaldinho asaini kadi yake ya njano
Post a Comment