Thursday, 25 February 2016
Katekesi ya Papa : Utajiri na madaraka vyapaswa kuhudumia watu wote.
Posted by Unknown on 23:22:00 in | Comments : 0
Mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko , ya kila Jumatano kwa mahujaji na wageni, yameendelea kuizungumzia huruma ya Mungu katika huduma kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu. Papa amerejea Agano la kale akianisha na Agano jipya vifungu vinazungumzia nguvu za Utajiri, Ufalme, na wenye mamlaka ya juu , na pia ya kiburi cha majivuno na ukatili wao.
Baba Mtakatifu amekiri ukweli kwamba, utajiri na mamlaka vina nguvu ya kutengeneza mazuri lakini tu kama vitatumiwa kwa manufaa ya wote, hasa iwapo vitatumika kama huduma kwa haki na upendo kwa watu wahitaji, hasa maskini. Bahati mbaya aliendelea , uzoefu mara nyingi umeonyesha utendaji tofauti na huo, utajiri ukitumika kama nafasi ya kutoa upendeleo kwa wenye navyo matajiri , na kujenga hali ya kugandamiza wasiokuwa navyo, ubinafsi na nguvu na hata kusababisha uwepo wa rushwa na hata mauaji, kama ilivyotokea katika shamba la mizabibu la Nabothi, ilivyoelezwa katika kitabu Kwanza cha Wafalme Sura ya 21, ambamo Naboth ,anatendewa kinyume cha haki, kunyang’anywa shamba lake na kuuawa ili Mfalme Ahab , amiliki aridhi yake.
Papa alitazama kwa kina maelezo hayo na kusema kuwa Yesu leo hii anatutaka kuwa tofauti na roho hiyo, anatutaka kuonyesha ukuu si kwa kugandamiza, lakini kwa unyenyekevu wa kujaliana mmoja kwa mwingine. Alieleza kwa kurejea maneno ya Yesu, kwa wanafunzi wake alipowaonya wasitawale kwa kugandamiza lakini uwezo wa mamlaka na uongozi iwe ni huduma ” yeyote anayetaka kuwa mkuu kati yenu ni lazima awe mtumishi wenu, na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu lazima awe mtumwa wenu “(Mt 20.25-27). Papa amesema kwa mtawala anayepoteza mwelekeo wa huduma, basi nguvu yake humezwa na kiburi cha unyanyasaji kama kile kilichotokea katika shamba la mizabibu la Nabothi. Yezebeli, kwa njia za hila anaamua kumwondoa Nabothi ili atekeleze mpango wake dhalimu, wa mfalme kumiliki mali ya Nabothi. Huu ni ukaidi na majivuno ya mamlaka yasiyo heshimu maisha , ni utawala usiokuwa na haki wala huruma. Ni kiu ya kutawala wenye kujenga moyo wa uchoyo na ubinafsi wa kutaka kumiliki kila kitu. Lakini Bwana anaonya juu ya tamaa hizo za wenye mamlaka na matajiri, akisema , ole wenu ninyi mnaotaka kujiongezea utajiri wa nyumba hadi nyumba, kuongeza shamba hadi shamba, mpaka hakuna nafasi zaidi ya kukaa wengine na hivyo mnabaki peke yenu (Isa 5,8).
Na kwamba , Yesu anatuambia kwamba ni lazima kuonyesha ukuu wwetu si kwa klugandamiza wengine lakini kwa kutumikiana kwa unyenyekevu, mmojakw amwingine. Na kwama Bwana alivyomtuma Nabii Elia kumtaka Ahab atubu dhambi zake , pia alimtumwa mwana wake pekee kutuonyesha huruma yake ya kuokoa yenye kutuweka huru dhidi ya dhambi na ukosefu wa haki . Huruma huwa na uwezo wa kuponya dhambi n aina unaweza kubadilisha historia ya maisha yetu. Hurma ya Mungu ni nguvu kuliko dhambi ya binadamu. Nguvu ya Yesu yakuokoa huonekana katika mti wa Msalaba wa Yesu.
Papa alikamilisha na ombi kwamba, katika mwaka huu Mtakatifu, na tumwombe Bwana ajongee karibu zaidi wadhambi , na kutuonyesha huruma yake yenye kutukomboa katika hali nyingi za ukosefu wa haki katika dunia hii yetu, kwa uwezo wake huruma yake na msamaha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment