Thursday, 4 February 2016
Dunia yahaha na mfumko mpya wa virusi vya zika
Posted by Unknown on 00:40:00 in | Comments : 0
Baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza kuwa virusi vya Zika kuwa dharura ya kimataifa, shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeomba kiasi cha dola milioni tisa kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya zika , hasa barani Amerika ya kusini , ambako virusi hivyo vimeenea karibia katika nchi 25.
UNICEF imesema, kwa ajili ya Brazil, ugonjwa uliko shamiri zaidi , kwa kushirikiana na wadau wengine na jamii, ina mpango wa kutuma ujumbe wake kwa ajili ya kuhamasisha mwamko zaidi, katika jinsi ya kuepuka kung'atwa na mbu anayeeneza ugonjwa huo na kutokomeza masalia ya wadudu hao . Pia fedha hizo zitasaidia kupunguza makali ya madhara yake kwa watoto wachanga , familia na ukanda mzima wa Amerika ya Kusini. Christophe Boulierac , msemaji wa UNICEF Geneva , alieleza hilo wakati akikutana na wanahabari . UNICEF imesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua haraka na kuwapatia wanawake na wajawazito taarifa sahihi kwa ajili ya kujikinga na virusi hizo, vinavyoenezwa na mbu aina ya Aedes aegypti.
Nayo WHO inasema ingawa virusi vya Zika si kitisho katika ujauzito kama HIV au Ebola lakini athari zakepia ni kubwa kwa familia kwa kuwa husababisha ulemavu wa kudumu katika mishipa ya fahamu. Siku za nyuma haukuwa tatizo katika afya ya umma,lakini sasa umekuwa kitisho kutokana na wingi wa watoto, waliozaliwa na ulemavu wa akili katika mataifa ya Amerika ya Kusini, ambako Brazil peke yake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, Oktoba 2015 hadi Januari 2016, umesababisha watoto zaidi ya 4,000 kuzaliwa na kasoro katika mfumo wa mishipa ya fahamu.
WHO inapendekeza uwepo wa uratibu kimataifa, katika juhudi za kupunguza tishio hilo, hasa katika nchi zilizoathirika zaidi na pia kwa lengo la kupunguza hatari ya kuenea zaidi ya kimataifa. .
Kati ya njia zinazoweza kutumiwa kirahisi kujikinga na kuumwa na mbu mwenye virusi, ni kama ilivyo tu kwa aina nyingine za mbu , ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi yanayofunika mwili mzima, kuhakikisha mazingira ni safi na hakuna matuamo ya maji ambako mbu wanaweza zaliana. Kulala ndani ya vyandarua n.k. Na wanawake wajawazito ambao wanahisi kuwa na dalili za ugonjwa huo mara moja kupata huduma hospitalini.
Kitengo cha Afya ya Umma Kimataifa cha Shirika la Afya la Dunia (WHO), Jumatatu kilitangaza uwepo wa mfumko wa maradhi ya ubongo , unaosababishwa na virusi vinavyoitwa Zika vinavyoenezwa na mbu aina ya aedes aegypt. Aina ya virusi ambavyo siku z anyuma havikuwa kitisho kwa afya ya umma. Lakini kwa sasa vinatisha baada ya kuhusishwa na uwepo wa watoto wengi wenye kasoro katika mfumo wa mishipa ya fahamu , tatizo lililoonekana kwa wingi huko Amerika ya kusini.
Wataalam wa afya wanasema virusi hivyo vikimwingia mama mjamzito hushambulia kijusi cha mimba, na kama matokeo yake mtoto huzaliwa na kichwa kidogo kuliko kawaida na pia huleta kasoro katika ukuaji wa mfumo wa fahamu.
Wakati wanasayansi watafiti wakiendelea na kazi zao kwa ajili ya kukabiliana na virusi Zika , pia wanahoji kwa vipi virus hawa ambao uwepo wao ulijulikana tangu mwaka 1947, sasa wafumke kwa wingi?
Dr Anthony Fauci, Mkurugenzi katika taasisiya Kitaifa ya maradhi ya kuambukiza na uzio , amekiri kwamba, virusi Zika hawakuwa tisho la afya ya umma hadi mwaka 2013 , walipoanza kuonekana kwa wingi katika kisiwa cha Polynesia . Na mwaka 2015, watu zadi ya milioni moja na nusu walipatwa ambukizo la virusi hao , wakisababisha zaidi ya watoto elfu nne kuzaliwa na ulevu wa kichwa na ubongo wengi wao wakiwa Brazil.
Dalili za kushambuliwa na virus Zika zimetajwa kuwa ni pamoja na mgonjwa kuwa na homa kali, maumivu katika viungo vya mwili na mwili kutokwa na viji pele. Na kwamba, shambulio la virusi hao kwa kawaida halidhoofishi sana mwili kama ilivyo kwa homa zingine kama dengue na malaria.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment