BODI
ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi
Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha
uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba
amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na
kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo
ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.
“Kumekuwa
na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni
hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa
stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo
wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.
Aidha
Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo
na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji
mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.
Hatua
hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape
Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo
ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21
kuacha kazi.
“Nataka
Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue
hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua
mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.
Hata
hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha
utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji
wa magazeti kwa kiwango kikubwa.
Post a Comment