BREAKING NEWS

Tuesday, 26 January 2016

WHO: Kipindupindu kimeua watu 200 Tanzania





kipindupindu

Shirika la Afya la dunia, WHO, limesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Tanzania umesababisha watu 222 kufariki dunia ndani ya kipindi cha miezi sita.
Watu 14,003 wameugua kutokana na ugonjwa huo.
Mwanzoni wa mwezi wa Januari, Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi 11 zilizopewa chanjo kutoka kwa WHO.
Tangu Agosti, kipindupindu kimeripotiwa katika mikoa 27 nchini humo.
Japo Tanzania ilipokea chanjo kutoka WHO mwanzoni mwa mwaka jana, maafisa wa afya wa serikali wanasema chanjo hiyo haitoshi.
Hata hivyo, Wizara ya Afya ya Tanzania imesema kuwa vikosi kasi vya afya vimetumwa katika sehemu vya dharura, na kuongezea kuwa kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo imeanza kupungua.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree