BREAKING NEWS

Tuesday, 26 January 2016

Waliotia Matatu nakshi taabani Kenya









Magari mengi ya uchukuzi wa umma nchini Kenya yamekamatwa kufuatia msako mkubwa ulioanzishwa na mamlaka ya usafiri na usalama barabarani nchini Kenya, (NTSA).
Hii ni kufuatia sheria mpya inayozuia magari ya uchukuzi wa umma kuwa na rangi tofauti, michoro ya sanaa, honi zinazosababisha kelele na mziki wa sauti ya juu.
Kuna maelfu ya magari ya uchukuzi wa umma nchini Kenya yaliyopambwa na kuwekwa nakshi kinyume cha sheria na Mamlaka hiyo ya NTSA inasema kuwa hatua hiyo inalenga kuboresha usafiri wa umma.



Mamlaka hiyo ya usafiri inasema kuwa magari hayo yenye michoro na taa nyingi yanapaswa kuondolewa mabarabarani kwani yanahatarisha maisha ya waendeshaji wengine wa magari.
Magari hayo maarufu, kama matatu au matwana, ni maarufu miongoni mwa abiria wa usafiri wa umma nchini Kenya kwa sababu ya uwezo wao wa kupenya kwa njia za mkato ilikukwepa foleni.
Awali rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aliwaruhusu wamiliki wa magari kuweka michoro maandishi na nakshi lakini mamlaka hiyo imekwenda kinyume na agizo hilo ikidai kuwa inakiuka sheria za kulinda usalama wa barabarani.



 


Mwenyekiti wa NTSA Bwana Lee Kinyanjui ameiambia BBC kuwa magari mengi yamekiuka kibali cha rais na kukaidi maadili ya umiliki na uendeshaji wa magari.
''Magari mengi ya matatu yanakiukaji sheria za barabarani mbali na kuweka maandishi yasiyoruhusiwa,’’ alisema Kinyanjui .
''Baadhi yao yanacheza muziki kwa sauti ya juu bila kuelewa wanaharibu mazingira na kuathiri afya ya abiria ’’ Kinyanjui ameongeza
Magari hayo yanadaiwa kutoa ajira kwa mamilioni ya vijana nchini Kenya huku sekta hiyo ya usafiri wa umma ikiwa mojawapo ya tegemeo la wakenya wengi ambao yamkini hawakuwa na kazi kujitafutia riziki yao ya kilasiku.



’Biashara imeathirika kwa sababu magari yetu hayana mvuto, vijana wamezoea mziki na michoro ya kufana lakini leo, tumeathirika zaidi,’’ mmoja wa wahudumu wa magari hayo, Ismael Gaza alimwambia mwandishi wetu, Abdinoor Aden.
Operesheni hiyo inatarajiwa kuendelea hadi pale wamiliki a magari watakapotii sheria hizo mpya zinazowataka kuweka rangi chache tu mbali na nembo ya mashirika ya usafiri pekee kwenye magari hayo ya uchukuzi wa umma.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree