Waziri
mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa,amesema serikali imeweka
msisitizo katika kuhakikisha inarudisha nidhamu kwa watumishi wa umma
kwa kuweka mkazo katika uadilifu, uwajibikaji, kutoa huduma kwa wakati.
Waziri
mkuu Majaliwa ameyasema hayo katika mkutano wa pili kikao cha tatu
Bungeni Mjini Dodoma alipokua akihitimisha hoja ya kujadili hotuba ya
Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja
tarehe 20 Novemba 2015
Amesema
kuwa serikali itakuwa inawakumbusha watanzania na watendaji wa
serikali kufanya majukumu yao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuchukua
hatua za haraka dhidi ya watumishi wanaokwenda kinyume na misingi ya
utendaji kazi serikali kwa kuzingatia kauli mbiu ya hapa kazi tuu.
Pia
amesema kuwa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge ambazo utekelezaji
wake utahitaji kutengewa fedha za uandalizi wa kutenga fedha za serikali
na utendaji wake utafanyika kwa haraka kwa kuzingatia maombi na hoja za
wabunge kwakusimamia mapato ya Taifa ili yaongezeke kwa kiwango
kikubwa.
Post a Comment