Michango ya wabunge katika kuijadili hotuba ya Rais JPM
SERIKALI imeshauriwa kuwasilisha Bungeni sheria
zote zinazokinzana na kasi ya Rais Dk. John Magufuli ya kufanya mabadiliko ya
haraka ya kiutendaji, hapa nchini.
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe,
alisema hayo jana, Bungeni mjini hapa, wakati akichangia hotuba ya rais.
Alisema kuna malalamiko mbalimbali kuwa kasi ya
rais, inayofanyika hivi sasa, imekuwa ikipingana na baadhi ya sheria za nchi.
Bashe alisema baadhi ya sheria, zilizopo hivi sasa
zimekuwa ni kichaka kikubwa cha wezi wanaoliibia taifa.
Alisema sheria kama ya manunuzi ni sheria ambayo
imekuwa ikitoa mwanya kwa watumishi kuibia nchi.
“Utaona kuwa kwa kutumia sheria hiyo, choo kina
jengwa kwa sh. milioni 20, kwa kutumia sheria hii ya manunuzi kupitia
makandarasi wakati choo hicho hata milioni tano hakifiki,’’ alisema.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, kunahitajika kiongozi
kama Rais Magufuli katika kufanya maamuzi sahihi ili jamii iweze kuondoka hapa
ilipo na kupiga hatua.
“Watu wanahoji eti kwanini serikali imetoa fedha
na kupeleka mashuleni bila kupitia bajeti ndogo sasa ulitaka watoto wetu
wasiende shule,’’ alisema.
Aliongeza kuwa “Tunahitaji rais wa aina hii, kwa
sasa akanyage sheria ili mambo yaende na kama zipo sharia mbovu basi ziletwe
hapa tuzifute,’’ alisema.
Aidha mbunge huyo, aliiomba Wizara ya Fedha na
Mipango, kuhakikisha inatenga fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa reli kwa
ukubwa wa (Standard Gauge).
Alisema reli ni moja ya njia muhimu ya kusafirisha
mizigo mbalimbali ikiwemo hata ya nje ya nchi.
Kwa upande wake, Dk.Pudensiana Kikwembe
(Kavuu-CCM), alisema suala la elimu bure ni muhimu likatolewa ufafanuzi zaidi
kwa sasa.
Alisema kumekuwa na sitofahamu miongoni mwa
watendaji wanaotekeleza sera hiyo kwani bado kuna changamoto nyingi.
“Nawaomba walimu wakuu kutumia fedha hizo kwa
minajili iliyokusudiwa na si vinginevyo,” alisema.
Naye, Agustine Masele (Mbogwe-CCM) aliwataka
Watanzania kumuombea Rais Magufuli kwa kazi nzito anayoifanya ya kutumbua majipu.
Alisema hivi sasa taswira ya nchi imeanza
kuonekana kutokana na majipu kutumbuliwa kila kukicha.
Akizungumzia viwanda, mbunge huyo alisema ni
muhimu viwanda vikafufuliwa ili kuongea ajira kwa wananchi walio wengi.
Wizara ya Maliasili na Utalii
WIZARA ya
Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi imeandaa mpango wa kupima maeneo yote
ambayo yana migogoro baina ya wananchi na hifadhi nchi nzima katika kipindi cha
mwaka 2015/ 16
Kauli hiyo
ilitolewa bungeni mjini hapa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa
Jumanne Magembe wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vitimaalum,
Ferister Bula(CCM),aliyetaka kujua ni lini serikali itamaliza mgogoro huo
utamalizika kati ya wananchi na hifadhi ya Mkongonelo iliyoko wilayani Kondoa mkoani
Dodoma.
“Hifadhi ya
Mkongonelo, wananchi wameuwawa na askari wameuwawa, pale wananchi wanaomba
kilomita 50 tu ili mgogoro uishe lakini bado ni tatizo mpaka leo,” alisema.
Katika swali
la msingi Mbunge wa Vitimaalum, Cecilia Paresso(Chadema),alitaka kujua ni lini
matokeo ya kamati ya ndogo iliuoundwa na aliyekuwa waziri wa maliasili na
utalii, kwa ajili ya kushughulikia mgogoro uliopokati ya wananchi na hifadhi wa
kata ya Bunger na hifadhi ya Taifa ya Manyara.
Pia alitaka
kujua ni lini wananchi watapewa taarifa ya kamati hiyo.
Akijibu
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Ramo Makani, alisema taarifa ya Tume
imebaini kuwa , kwa ujumla chanzo kikubwa cha mogogoro baina ya wananchi na
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
“Ni idadi
kubwa ya mifugo na kukosekana eneo la kuchungia katika kijiji cha Buger, Tume
imependekeza hatua mbalimbali za kuchukuliwa,” alisema
Alizitaja
hatua hizo kuwa ni pamoja na za kuchukuliwa ambazo ni pamoja na kufanya sense
ya mifugo kwa vijiji vilivyopo katika kata ya Buger ili kubaini idadi ya mifugo
iliyoko dhidi ya ukubwa wa ardhi waliyonayo.
Nyingine ni
Vijiji kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi, kutoa elimu ya uhifadhi na sheria
katika vijini na kuimarisha zilizopo ili kutelekeza vema majukumu yake.
Aliitaja
hatua nyingine kuwa ni TANAPA kuweka nguvu kuchangia miradi ya maendeleo ya
maendeleo ya jamii kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi.
Naibu Waziri
huyo Wizara itaandaa kikao cha wadau ndani ya miezi mitatu ili kuwasilisha
mapendekezo ya kamati na kujadili utekelezaji wake.
Tamisemi
SERIKALI
imesema bado haijakamilisha mchakato wa kuanzishwa mkoa wa Songwe haujakamilika
kwa kuwa bado hawajatoa tangazo maalum kwenye gazeti la serikali.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene, aliliambia bunge mjini hapa
jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mombo, David Silinde(Chadema), aliyetaka kujua kwanini
serikali inakuwa na kigugumizi katika kufanikisha uanzishwaji wa mkoa wa Mombo.
Waziri huyo
alimtaka mbunge kuvuta subira wakati ukifika watakapokamilisha mchakato wote
watatoa tangazo maalum la Rais kuanzisha mkoa mpya wa Mombo.
Aidha
Serikali, imetenga Sh. milioni 282.7 kwa ajili kuendeleza ujenzi wa nyuma hizo
na Sh. milioni 200.0 zimetengwa kuanza ujenzi wa Ofisi ya Mkuu ya mkuu wa
Wilaya.
Hayo
yalieleze bungeni mjini hapa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI,
Seleman Jaffo, wakati akijibu swali la msingi la Silinde,(Chadema).
Katika swali
lake Mbunge huyo, alitaka kujua ni kwa nini serikali imekuwa ikisuasua kautoa
fedha ili ziweze kujenga Ofisi na Nyumba za watumishi katika makao makuu ya
wilaya Mombo eneo la chitete.
Jaffo
alisema serikali katika mwaka wa fedha 2013/24 ilifanikiwa kupeleka Sh. milioni
250.0 ambazo zimetumika kuanzia ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya katika mwaka
wa fedha 2014/15 fedha zilizotengwa kwa kazi hizo hakupelekwa.
Alisema kwa
upande wa ujenzi wa Ofisi za halmashauri ya wilaya ya Momba, serikali katika
mwaka 2014/15 ilitoa Sh. milioni 450 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi hizo.
“Katika
jitihada ya kuhakikisha halmashauri inawapatia watumishi wake nyumba bora,
serikali imezielekeza halmashauri kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi
wa nyumba za watumishi.
Wizara ya mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa
WAZIRI wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Harson
Mwakyembe amesema serikali haina taarifa za kuwepo kwa watanzania wanaofanya
biashara nje ya nchi ambao walipata matatizo nchini Kenya na kukosa msaada
kutoka ubalozi na wizarani.
Aidha
alimtaka, mbunge kupeleka taarifa katika wizara hiyo kama kweli kuna taarifa
hizo mana ni nzito ili ziweze kufanyiwa kazi.
Mwakyembe, alikuwa
ajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Micheweni, Haji Khatibu Kai(CUF),
aliyetaka kujua ni kwanini watanzania zaidi ya 100 wa jimbo la Kai walipopata
matatizo nchini Kenya hawakupatiwa msaada licha ya kutoa taarifa ubalozi na
wizarani.
Aidha,
Waziri huyo licha ya kukiri kutokuwa na taarifa hizo na kumtaka mbunge
kuwapelekea kwa maandishi, alitoa wito kwa wananchi wa Tanzania wanaofanya
biashara nje ya Nchi kutoa taarifa ubalozi ili wanapopawa na matatizo ili
wapatiwe msaada wa haraka.
Katika swali
la msingi mbunge huyo alitaka kujua, serikali inawashauri nini wananchi wake
wanaokwenda kibiashara kwenye nchi zinazounda umoja wa Afrika Mashariki.
Pia alitaka
kujua wananchi hao wanapaswa kupeleka malalamiko yao wapi pindi wanapopata
matatizo au vikwazo wawapo nje ya nchi.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Suzan Kolimba, alisema nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeondolewa ushuru wa forodha mipakani.
Dk.Suzan
alisema, hatua hiyo inapanua soko la bidhaa za Tanzania kufikia wanaafrika Mashariki
takribani milioni 143 katika nchi tano wanachama wa Jumuiya za Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burudan.
“Ni dhahiri
kuwa endapo soko hilo litatumika kikamilifu litachangia kwa kiasi kikubwa
kukuza uchumi wa Taifa na kupunguza umaskini wa wananchi wetu,” alisema.
Alisema,
serikali inawashauri wananchi kuzichangamkia fursa za kibiashara, ajira,
uwekezaji zitokanazo na Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kujiharakishia maendeleo.
Mwisho

Katiba na sheria

Post a Comment