BREAKING NEWS

Saturday, 30 January 2016

Watumishi wa Afya kuweni wabunifu katika utoaji huduma kwa jamii

Watumishi wa sekta ya afya watakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu


Hayo yamesemwa leo na Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,dkt. Hamisi Kigwangwala wakati akitembelea hospitali ya mount meru mkoani arusha

Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe Kwa ukusanyaji was mapato,hivyo ipo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao utawafanya watu Wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi

"Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapo

Aidha,dkt.kigwangwala alisema licha ya serikali kupata pesa,watoa huduma pia wakiwemo madaktari,wauguzi pamoja na kada zingine kupata motisha ambazo zitawafanya kuwapa moyo wa kuwahudumia wagonjwa law hali na Mali.

"Kama matajiri hawaji kwenye hospitali Za umma,mnategemea hawa maskini watapata pesa wapi za kulipia huduma?aliuliza.

Hatahivyo naibu waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma Kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma,dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko pa kulipia

"Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma Za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma was serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree