
Baada ya kusimama Ligi Kuu kwa wiki moja ili kupisha mechi za Kombe la
FA, Ligi Kuu
Tanzania bara mzunguuko wa pili umeanza kwa vilabu vya Ligi Kuu kurudi uwanjani leo January 30, uwanja wa
Taifa Dar Es Salaam, Simba walikuwa wenyeji wa
African Sports wakati ambao watani zao wa jadi
Yanga walikuwa
Tanga kucheza na
Coastal Union.
Simba walikuwa uwanja wa
Taifa kurudiana na
African Sports ambao mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliochezwa uwanja wa
Mkwakwani Tanga September 12 2015 waliwafunga kwa goli 1-0. January 30 2016
African Sports walirudi tena kuvaana na
Simba katika mchezo wa mzunguuko wa pili na kuchezea kichapo.
African Sports wameendeleza kuwa vibonde wa
Simba baada ya kukubali kipigo cha goli 4-0, magoli ya
Simba yalianza kufungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa
Uganda Hamis Kiiza dakika ya 14,
Hassan Kessy dakika ya 31 na dakika ya 43
Hamis Kiiza alifunga goli la tatu kwa
Simba, kabla ya
Haji Ugando hajapachika goli la nne dakika ya 75 kipindi cha pili.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa January 30
- Coastal Union 2 – 0 Yanga
- JKT Ruvu 0 – 0 Majimaji FC
- Mwadui FC 1 – 0 Toto Africans

Post a Comment