Timu
ya Kenya ya mchezo wa raga imeicharaza Canada na Ureno 37-7 na 26-5 ili
kufika katika robo fainali ya Kombe la Wellington Sevens siku ya
jumamosi nchini New Zealand.
Hatahivyo,Kenya ilipoteza mechi yake ya tatu kwa Australia baada ya kufungwa 17-12 katika mechi ya kundi Da.
Wachezaji
wa kocha Benjamin Ayimba sasa watakabiliana na wenyeji New Zealnd
mapema siku ya jumapili katika robo fainali ya taji kuu.
Australia awali ilikuwa imeishinda Ureno 19-12 na Canada 26-22.
Trai za
Collins Injera na Billy Odhiambo, konvashon iliofungwa na Biko Adema
iliisaidia Kenya kuongoza dhidi ya canada 12-0 ifikiapo kipindi cha
mapumziko.
Post a Comment