Congo imepata goli lake kunako dakika ya 11 kupitia mchezaji wa kiungo Doxa Gikanji aliyekunjua shuti kutoka mita 18.
Wachezaji
wa Rwanda hawakutarajia goli hilo na wameonekana kukatishwa tamaa na
goli hilo la mapema mbele ya mashabiki wao zaidi ya elfu 20 waliojazana
kwenye uwanja wa taifa Amahoro.
Congo ilitawala kipindi cha kwanza kwa chenga,pasi na mbwembwe za kila aina. Kipindi cha pili mambo yalibadilika
Dakika ya
24 nusura Congo wapate goli la pili.Mpira uliopigwa ghafla na
mshambuliaji Elia Meschack ulirudishwa na mlingoti wa lango.(VICTOR)
Nafasi
pekee ya kutishia lango la Congo ilikuja kwenye dakika ya 37 mpira
uliopigwa na mshambuliaji Jacques Tuyisenge ulilazimisha kipa wa Congo
kufanya kazi ya ziada kuokoa jahazi lake.
Katika
kipindi cha pili Rwanda ilikuja juu na kutawala mchezo hadi dakika ya 57
ilipoandikisha goli la kusawazisha kupitia mshambuliaji Ernest Sugira.
Hadi dakika 90 kumalizika matokeo yameendelea kuwa hayo.
Goli la
ushindi la Congo lilipatikana kwenye dakika ya 114 kupitia mchezaji
Botuli Bompunga,aliyiwezesha Congo kutinga nusu fainali.CHANZO:BBC
Post a Comment