Katika hatua ya kujumuisha umoja wa
kikristo,Papa Francis amewaomba radhi waamini wa kiprotestanti kutokana
na historia ya unyanyasaji walioupata kutoka kanisa katoliki.
Hata
hivyo Papa Francis amewataka waamini wa kanisa katoliki pia kuwasamehe
wale ambao waliwakosea ili wasiruhusu makosa yaliyotendeka nyuma kuwa
sumu ya mahusiano ya sasa.Kufuatia tamko hilo msemaji wa Vatcan ametangaza kuwa Papa Francis atazuru mji wa Lund uliopo Swedish eneo ambalo jumuiya ya kilutheli ilianzishwa na kuanzisha thehebu la kilutheri karne tano zilizopita.
Post a Comment