BREAKING NEWS

Tuesday, 26 January 2016

Niyonzima kavuliwa unahodha msaidizi Yanga? kwa nini hakuvaa beji FA Cup? majibu yapo hapa

Jumapili ya January 24 klabu ya Dar Es Salaam Young African ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa Kombe la FA dhidi ya Friends Rangers, lakini huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea klabu hiyo Haruna Niyonzima kurejea uwanjani toka amalizane na uongozi kuhusu matatizo yake.
Stori au jambo lililovuta hisia za watu wengi ni kuhusiana na Haruna Niyonzima kutovaa beji ya unahodha ambayo, yeye alistahili kuvaa, badala  ya Vicent Bossou kwani ndio nahodha msaidizi, mara nyingi kama Canavaro hayupo yeye huwa anavaa, Amplifaya ya Clouds FM ilifanya exclusive interview na Haruna Niyonzima juu ya suala hilo. Kavuliwa unahodha?

niyonzima 

Siwezi kulizungumzia nimetoka kwenye matatizo kikubwa ni nimerudi kazini, kuhusu mshahara wa nyuma bado sijalipwa ila nitalipwa kwani ipo kwenye mchakato, nikiwa nimetoka kwenye matatizo yangu ni ngumu kuliweka akilini suala la kuwa unahodha, hivyo mwali anaweza kumchagua mchezaji yoyote atuongoze kwani sisi sote ni manahodha na familia moja akivaa yoyote sawa tu” >>> Niyonzima

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree