Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine
leo amefungua kozi ya ngazi ya juu ya ukocha kwa wanawake (High Level
Coaching Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.
Akiongea
na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Mwesigwa
amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia mafunzo hayo na kuitumia
vyema fursa hiyo adimu waliyoipata.
Mwesigwa
amewataka washiriki kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano, inawasaidia na
kwenda kuwa walimu wa mpira wa miguu kwa wanawake, na kuongeza mwamko
kwa wanawake wengi kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.(VICTOR)
Aidha
Mwesigwa, amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo ya
mkufunzi, nidhamu ya ndani na nje ya uwanja kwani imekua ni bahati nzuri
kwao kupata nafasi ya kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.
Naye
mkufunzi wa kozi hiyo anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni amesema
atatumia uwezo wake wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo wanajifunza
na kuelewa vizuri mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu wazuri
watakapokwenda kuanza kufundisha.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma ameishukuru TFF kwa
kuendesha kozi hiyo na kusema kupatikana waalimu wengi wa kike
kutaongeza mwamko wa wanawake kuucheza mpira wa miguu.
Jumla ya
washiriki 25 wanashiriki kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao
ni Fatuma Omary, Esther Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie Charles, Pendo
John, Berlina Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth Sokoni, Sophia
Mkumba, Marry Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.
Wengine
ni Veneranda Mbano, Mariam Aziz, Hilda Masanche, Chichi Mwidege, Sophia
Edward, Asha Rashid, Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu Muharami, Tatu
Malogo, Komba Alfred, Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na Ingfridy
Kimaro.
Post a Comment