BREAKING NEWS

Wednesday, 27 January 2016

Mugabe akemewa kwa upendeleo makaburini

                        
Upinzani nchini Zimbabwe umekishtumu chama cha rais Robert Mugabe ZANU PF kwa kubadilisha makaburi ya mashujaa ambapo viongozi wakuu waliopigana dhidi ya uongozi wa mweupe walizikwa kuwa mahali patakatifu kwa wanachama wa ZANU PF kulingana na chombo cha habari cha AP.

''Tumekubali kwamba hili ni eneo la makaburi la chama cha ZANU PF,lakini utumizi wa fedha za uma kulipia eneo hilo ni uhalifu,''. Alisema Luke Tamborinyoka,ambaye ni msemaji wa chama cha MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai.
AP imeripoti kwamba afisa wa MDC Alex Musundire na wakili Tinomudaishe Chinyoka waliwasilisha kesi katika mahakama ya kikatiba wakimshtumu rais Mugabe kwa kukosa kufuata sheria wakati anapoamua ni nani anayefaa kuzikwa katika makaburi hayo ya mashujaa katika mji mkuu wa Harare.
Pia wamemshtumu Mugabe kwa kuwa na upendeleo,kufuatia kuzikwa kwa dadaake katika eneo hilo,AP imeongeza.
''Sabina Mugabe ..hana kumbukumbu katika serikali yoyote ama chapisho lolote ninalolijua kwa kuwa hajafanya lolote kijulikanacho'',Bwana Chinyoka alinukuliwa akisema.
Katika hotuba aliofanya katika makaburi hayo ya mashujaa mwaka uliopita,Mugabe mwenye umri wa miaka 91 alisema;''Wenzangu waliokosa mwelekeo wana maoni finyu kuhusu ni nani anayefaa kutangazwa kuwa shujaa''.
''Wacha niweke wazi kwamba maeneo haya matakatifu ni ya mashujaa wetu pekee waliopigania uhuru wa taifa hili'',aliongeza.
Mashujaa waliopigana na ukoloni na ambao walizikwa katika Heroes Acre ni makamu wa rais Joshua Nkomo na mkuu wa majeshi Solomon Mujuru.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree