Klabu ya Chelsea ya Uingereza January 30 imeingia kwenye headlines za usajili wa beki wa kati, baada ya dalili za kumpata beki wa Everton John Stones kuwa ndogo, kwani wamewahi kuomba kumsajili kutokea klabu yake ya Everton kwa zaidi ya mara tatu licha ya kujitahidi kuongeza dau mara kadhaa.
January 30 klabu ya soka ya Chelsea imetangaza kumsajili beki wa kati wa klabu ya New York Red Bulls ya Marekani Matt Miazga, beki huyo amesaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuitumikia klabu ya Chelsea, ambapo dalili zinaonesha Chelsea inatafuta mrithi wa John Terry kwa miaka ya baadae.
Matt Miazga mwenye umri wa miaka 20, amesajiliwa kwa dau la pound milioni 3.5. Miazga anatokea New Jersey Marekani, lakini hakusita kueleza furaha yake ya kujiunga na Chelsea “Nina furaha kujiunga na Chelsea, klabu ambayo ni maarufu duniani na ina mafanikio makubwa”
Post a Comment