BREAKING NEWS

Wednesday, 27 January 2016

Denmark na sheria tata ya wahamiaji


Umoja wa mataifa umekosoa hatua iliyochukuliwa na bunge Danmark kupitisha sheria yenye utata ya inayojaribu kuwazuia wahamiaji kuingia katika taifa hilo.
Sheria hiyo inatoa ruhusa kwa mamlaka ya serikali kutaifisha baadhi ya mali za wahamiaji wapya ili kufidia gharama ya huduma watakazopata.Sheria hiyo pia inalazimisha wakimbizi kusubiri hadi miaka mitatu kabla ya kuleta familia zao nchini nchini Denmark.
Upigaji kura umekamilika, 81 wamepiga kura ya ndio na 27 wamepiga kura ya hapana kukataa muswada, kura moja imeharibika, mswada umekubaliwa na sasa utapelekwa kwa Waziri Mkuu.
Mbali na kuzuiwa kuingia nchini Denmarka sasa wakambizi watakaopenya na kuingia nchini humo sasa ni ruksa kwa serikali kutaifisha mali zao kwa lengo la kufidia gharama za kuwahudumia.
Aidha wakimbizi waliobahatika kuingia hawataruhusiwa kuleta familia hadi miaka mitatu itimie.

Stephane Dujarric ,Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon wamepinga sheria hiyo ambapo amesema wakimbizi wanaokimbia vita na kuhatarisha maisha yao ili kufikia Ulaya, wanapaswa kuhudumiwa kwa moyo wa huruma.
"Nafikiri watu wanaoteseka, ambao wamekimbia vita na migogoro, ambao wametembea kwa miguu kwa mamia ya kilometa na zaidi na kuweka maisha yao hatarini kwa kuvuka bahari ya Mediterranean, wanapaswa kuhudumiwa kwa moyo wa huruma na kuheshimiwa utu wao ikiwa ni pamoja na kupewa haki zote za ukimbizi wanazostahili."
Mmoja ya wakimbizi wa Syria anayeishi Denmark Mohamed ameimbia BBC kuwa hatua hiyo mpya ina lengo la kutimiza azma yao.
"Siwezi kumshauri mtu yeyote kuja hapa Denmark. Nafikiri hivyo ndivyo serikali ya Denmark walivyotaka kueleza kuwa mtu yoyote kutoka nje ya nchi hiyo asije Denmark. Kusema ukweli hawataki watu zaidi kuja Denmark, na ninafikiri azma yao imetimia kwa sasa."
Kwa upande msemaji wa serikali ya Denmark Marcus Knuth , yeye amepongeza uamuzi huo wa bunge.
""Kama tulivyotarajia sheria hii imepitishwa na zaidi ya robo tatu ya wabunge, kwa sababu ni hatua muhimu itakayoifanya Denmark ifanane na nchi nyingine za bara la ulaya ili tusiwe moja ya nchi inayowapokea wakimbizi kutoka mbali, ikilinganishwa na ukubwa wa nchi yetu ambayo inapendwa na wakimbizi

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree