Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki-moon, amewaambia viongozi wa Afrika kwamba anaunga mkono pendekezo
lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka amani huko Burundi.
Alisema hayo katika mkutano wa viongozi wa nchi za AU nchini Ethiopia, ambako viongozi hao watapiga kura kuunga mkono au kukataa pendekezo hilo.
Rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amelipinga pendekezo hilo - Burundi inasema kutuma wanajeshi huko itaonekana kama uvamizi.
Uamuzi wa rais huyo kugombea muhula wa tatu wa uongozi ndiyo uliozusha ghasia za miezi kadha.
Kiongozi wa Gambia, Yahya Jammeh, ambaye alinyakua madaraka kwa kupindua serikali, alisema hatounga mkono pendekezo hilo iwapo Burundi haitoridhia.
Na rais wa Chad, Idris Deby, amepokea nafasi ya uenyekiti wa AU kutoka kwa kiongozi wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Post a Comment