Monday, 2 May 2016
Upande wa Pili wa Mkasa wa Ndoa ya Tiwa Savage Wawa Gumzo
Posted by Unknown on 12:37:00 in | Comments : 0
Mume wa Tiwa Savage, Tee Billz alipost mfululizo wa malalamiko kwenye Instagram kuhusu kumtuhumu mke wake kuwa alimsaliti na Doj Jazzy, Dr Sid na 2Face Idibia.
Jamaa huyo alionesha nia ya kutaka kujiua kutokana na masahibu hayo. Hiyo ilipelekea jamii kubwa ya Nigeria imchukie Tiwa kwa kumuona kama mwanamke katili na anayemtesa mumewe. Lakini upande wa pili wa shilingi wa mkasa huo unaweza ukabadili mawazo yako.
Kwa mujibu wa Tiwa, mume wake ndiye mzinguaji mkubwa na ana vimbwanga haswaa.
Akiongea kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote pale alipolazwa hospitali nchini Jamaica alikoenda kufanya video na Busy Signal.
Anasema wakati anajiandaa kwenda kushoot, alianza kutoka damu nyingi ukeni kiasi cha kupoteza fahamu. Alimpigia simu na kumtumia ujumbe mumewe ikiwa pamoja na kumtumia picha akiwa hoi kitandani lakini hakujibiwa hadi anatoka hospitali.
Siku amerejea Nigeria na akiwa amelala usiku wa saa nane, simu ya mumewe iliita kwa namba iliyohifadhiwa kwa jina la biashara lakini alishangaa iweje kampuni impigie usiku huo. Anadai alichukua simu ya mumewe na kuanza kusoma ujumbe wa WhatsApp na ndipo alipogundua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke na maongezi yao yalionesha kuwa walikutana hotelini na kufanya mapenzi. Kutokana na kitendo hicho aliondoka na kwenda kwa rafiki yake.
Anadai kuwa amekuwa akificha kwa muda mrefu kuhusu mume wake, lakini amedai tangu mtoto wao azaliwa, hajawahi kutumia hata senti kwaajili ya familia yao kwamba Tiwa ndiye kila kitu.
Amesimulia pia jinsi ambavyo mume wake amekuwa na tabia ya kumzunguka kwenye malipo ya show zake ambapo ametolea mfano wa harusi aliyotakiwa kwenda kutumbuiza London. Anasema alibaini kuwa mumewe alilipwa gharama zote lakini hadi anaenda kutumbuiza alimueleza kuwa hakuwa amelipwa. Kwakuwa alikuwa anafahamiana na miongoni mwa waandaji wa harusi hiyo alimuuliza na kujibiwa kuwa walikuwa wameshamlipa mume wake hela yote, miezi minne nyuma.
“Unamuibia mke wako, na yeye haoni kama ameniibia mimi, kwahiyo ilibidi nitumbuize kwenye harusi bure, kwasababu alikuwa ameshatapeli hela na sijui alizifanyia nini,” anasimulia.
Kwa upande mwingine staa huyo alieleza jinsi ambavyo mume wake alikuwa akiishia maisha ya zaidi ya kipato chake na hivyo wakati mwingine kumfanya ajikute kwenye madeni makubwa ambayo alilazimika kuyalipa.
Tiwa anasema jambo ambalo mume wake alizingua zaidi na ambalo limesababisha mgogoro wao ni pale alikopa naira milioni 45 ambazo ni sawa na shilingi milioni 495 za Kitanzania na kuchikichia. Kwa hali hiyo Tiwa alianza kuhofia usalama wake kwamba wanaomdai mumewe wangeweza hata kumdhuru ama kumteka yeye na mwanae kwasababu ya deni hilo.
Pia Tiwa amezungumzia jinsi ambavyo aligundua mume wake anatumia cocaine kitu ambacho kilimuumiza sana.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alikanusha kwa msisitizo kuwa hajawahi kamwe kumsaliti mume wake na Don Jazzy, Dr Sid wala 2Face na kwamba yupo tayari hata kuwekewa kifaa cha kubaini kama anasema uongo.
Mpaka hapo Tiwa ameonesha nia ya kuachana na mume wake, kitu ambacho anadai hakupenda kiwe.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment