Monday, 4 April 2016
Freeman Mbowe, Halipwi Mshahara Wowote na Chama Wala Posho
Posted by Unknown on 05:44:00 in | Comments : 0
Baada ya wengi sana jana kuhoji mshahara wa mwenyekiti wa chadema .mh freeman mbowe kufuati mh rais kutaja mshara wake. HILI NDIO JIBU LAKE
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe halipwi mshahara wowote na Chama. Amekitumikia Chama kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 20 akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu tangu aliposhiriki kuasisi Chama 1992, Mwenyekiti wa Vijana Taifa na baadaye Mwenyekiti wa Taifa kuanzia mwaka 2004.
Mbali na mshahara, Mbowe halipwi posho wala stahiki ya aina yeyote kama gari, nyumba, mawasiliano n.k na Chama. Utendaji wake ndani ya Chama ni wa kujitolea na kutoa.
Utamaduni huu umejengwa na viongozi wengi ndani ya Chadema kuanzia ngazi ya juu hadi chini.
Wanaolipwa posho ni watendaji wachache wanaofanya kazi full time katika ngazi ya Taifa na Kanda. Wabunge na madiwani wote walio na wadhifa wowote ndani ya Chama au katika Mabaraza yake nao hujitolea kwa asilimia 100 kwa kila namna watendapo majukumu yao ndani ya Chama. Hawapokei mishahara wala posho mbili mbili.
Hivyo Mbowe na viongozi wenzake wengi wa ngazi mbalimbali hawalipwi na Chama bali wao hukigharamia Chama kiweze kukua na kutekeleza majukumu yake kadiri iwezekanavyo.
Chanzo : Afisa habari Chadema
. Tumaini Makene
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment