Kwa kipindi cha hivi karibunin kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.
Tuhuma
hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari
baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale
zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi na kinaunga
mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.
Lazima
ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na
kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa
taifa.
CCM
inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia
hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya
rushwa.
Chama
cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za
kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya
rushwa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )