Wagombea wanaowania kupeperusha
bendera za vyama vya Republican na Democratic katika uchaguzi wa urais
Marekani wanajiandaa kwa siku muhimu sana uchaguzi wa mchujo, siku ya
Jumanne Kuu.
Majimbo 12 yatafanya mchujo siku ya leo kwenye kinyang’anyiro ambacho kitaamua hatima ya wagombea.Majimbo hayo ni kuanzia Massachusetts mashariki hadi Alaska kaskazini magharibi.
Baada ya mchujo kufanyika katika majimbo manne, Donald Trump anaongoza upande wa Republican naye Hillary Clinton upande wa Democratic.
SenataTed Cruz anahitaji kumshinda Bw Trump jimbo Texas, jimbo lake la nyumbani.
Bw Trump naye anahitaji sana kushinda Massachusetts, jimbo lenye wapiga kura wengi wa msimamo wa kadiri.
Bi Clinton anatumai ataweza kuendeleza ushindi wake, baada ya kushinda jimbo la South Carolina wikendi. Katika jimbo hilo, alipata kura nyingi kutoka kwa Wamarekani weusi baada ya kushindwa mchujo uliotangulia jimbo la New Hampshire na mpinzani wake mkuu Bernie Sanders.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika tarehe 8 Novemba kumchagua mrithi wa Rais Barack Obama ambaye ni wa chama cha Democratic.
Chini ya uongozi wa Rais Obama, chama cha Republican kimefanikiwa kutwaa udhibiti wa mabunge yote mawili ya Congress.
- Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
- Trump aahirisha ziara yake ya Israel
- Trump: Sitaacha kuwania urais Marekani
Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia, Alaska na Minnesota.
Kampeni ya mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York imewagawanya wanachama wa Republican.
Mkesha wa mchujo wa Jumanne Kuu, seneta wa Nebraska Ben Sasse alisema hatamuunga mkono Bw Trump.
Waandamanaji, baadhi kutoka kundi la kutetea haki za watu weusi la Black Lives Matter, walitatiza mikutano ya kampeni ya Trump Radford, Virginia, Jumatatu baada yake kukosa kushutumu kiongozi wa kundi la Ku Klux Klan linalotetea ubabe wa Wazungu, kwenye mahojiano.
Marco Rubio, mgombea wa Republican anayeshikilia nafasi ya tatu nyuma ya Bw Trump na Bw Cruz, anatumai ataweza kusalia kwenye kinyang’anyiro kwa kushinda jimbo lake la nyumbani la Florida tarehe 15 Machi.
Democrats watakuwa wakipiga kura Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia, Colorado na Minnesota, pamoja na eneo la American Samoa. Wafuasi wa Democratic nje ya nchi pia watapiga kura.
Bw Clinton anategemea kura za wapiga kura weusi maeneo ya Alabama, Georgia na Virginia baada ya kushinda asilimia 80 ya kura za watu weusi South Carolina.
Jane Sanders amesema mkewe anakabiliwa na changamoto Jumanne Kuu kwenye majimbo yatakayoshiriki mchujo lakini kwamba anatarajia kuendelea na kampeni hadi Julai wakati wa mkutano mkuu wa chama cha Democratic Julai.
"Tunatarajia kushinda baadhi ya majimbo na kushindwa majimbo mengie kes
Post a Comment