Mamlaka
ya Reli Nchini (TRL) imesitisha safari zake kutoka Dar es salaam kwenda
Mikoani na kuhamishia huduma hiyo mkoani Dodoma kutokana miundombinu ya
reli kuharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo
mbali mbali hapa nchini.
Mvua hizo zimeharibu miundombinu ya reli ya kati wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi TRL,
Masanja Kadogosa amesema kuwa kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo
ratiba ya huduma mpya inatarajiwa kuanza kesho Machi 22 kwa wasafiri
wanaotarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Kigoma kuanzia
majira ya saa 11 jioni.
Amesema
gari moshi jipya ya Delux kwa wasafiri wa Kigoma wanatakiwa kukata
stakabadhi ya malipo ya safari siku ya Jumanne saa 2:00.
Kadogosa
amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufuatia mashirikiano kati
ya kampuni hodhi ya Rahco pamoja na Shirika la reli nchini ili kuweza
kurejesha huduma hiyo kama ilivyokuwa awali.
Amesema
kuwa wasafiri wanaotumia usafiri huo waondowe wasiwasi kutokana na
jitihada zinazofanywa za urejeshaji wa huduma ya reli.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )