Friday, 25 March 2016
Pamoja na Operesheni 13, hii ni sababu inayomfanya Millen Magese asikate tamaa
Posted by Unknown on 20:11:00 in | Comments : 0
Kufanyiwa upasuaji mara 13 si kitu cha mzaha. Na tena kwa tatizo lenye maumivu makali kama la Endometriosis. Kipi kinachompa nguvu ya kuendelea kuinuka na kupaza sauti kuhusu tatizo hilo?
“Ninaamini kila mtu ana matatizo,” anasema Millen.
“Ukiyachukulia matatizo yako kuwa ni makubwa kuliko mwingine hilo linaweza kuwa tatizo kwasababu utakaa ndani utadhani kuwa ni wewe peke yako mwenye tatizo hilo. Kwangu mimi nimekaa na hili suala kwa miaka 23 mpaka naamua kuongea hili suala mwaka jana. Mimi kwanza nina familia yangu, wadogo zangu wananiangalia lakini kwa sasa nina zaidi ya familia, wasichana wadogo wananiangalia,” ameongeza.
“Ninajitahidi kuwaonesha kwamba chochote unachoumwa, tambua kuwa haupo peke yako. Na mimi kuwa nje kujaribu kuwa hai inanifanya nijisikie vizuri sababu inanifanya niwe hai tena. Nikiwa hivyo watu wanaoniangalia nao wanakuwa hivyo pia.”
Kwa sasa Millen anawaomba Watanzania kuendelea kumuunga mkono kwenye kampeni yake ya #13IsEnoughFindCure4Endo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment