Friday, 4 March 2016
Msieweke mafuta mkiwa na Abiria -- Mkuu wa Wilaya
Posted by Unknown on 10:59:00 in | Comments : 0
MKUU wa wilaya ya Monduli Francis Miti amewataka maderva hiace na waendesha magariya abiria kutokwenda katika vituo vya kuweka mafuta wakiwa wamebeba abiria.
Pia amewataka maderva wote na makondakta kufuata sheria za barabarani ikiwa ni pamoja na kuvaa sare na kutoa tikiti kwa abiria wote wanaosafiri kwenye magari yao.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Mto wa Mbu wilayani Monduli kufuatia kuwepo malalamiko kutoka kwa wananchi kwa madereva na makondakta wa magari ya abiria.
Miti amesisitiza kuwa hili ni suala la kisheria na yeyote atakayekiuka sheria itafuata mkondo wake ikiwa ni pamoja na hata kufutiwa leseni ya biashara kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha hali ya usalama kwa abiria.
Nao wananchi wliozungumza na Mwangaza FM wamesema kuwa imekuwa ni kawaida kwa makondakta kutotoa tikiti kwa abiria na madereva kupitishia abiria kwenye vituo vya kuweka mafuta wakati wanajua ni hatari.
Wameongeza kuwa wanapolalamika hutolewa lugha zisizofaa na kukasirishwa lakini kwa kuwa tayari wanakuwa wameshapanda gari wanavumilia ila kwa kauli ya mkuu wa wilaya wanaamimini itakuwa ni suluhu kwa tatizo hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment