Mahakamaa Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi ya baadhi ya
wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini ya kuruhusiwa kukata rufaa kupinga
uamuzi wa Makahama Kuu wa kufuta shauri lao la kupinga matokeo ya
uchaguzi.
Maombi hayo yaliwasilishwa na Magambo Masato na
wenzake wanne wanaompigania Stephen
Wassira, wakiiomba mahakama hiyo kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama
ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi
uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yaliyompa ushindi Ester
Bulaya (Chadema), dhidi ya Stephen Wasira (CCM).
Jaji
anayesikiliza shauri hilo namba 25 la mwaka 2016, Rose Ebrahim alisema
jana kuwa anakubaliana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi kuwa
hayana mashiko kisheria.
Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria.
Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria.
Wakili Marungu
alidai hati hiyo ilisaniwa na Wakili Denis Kahangwa na kuthibitishwa na
Wakili Constantine Mutalemwa kwamba hilo ni kosa kisheria, hivyo kuiomba
mahakama kutupilia mbali.
Akitoa uamuzi juu ya pingamizi hilo,
Jaji Ebrahim alisema anakubaliana na pingamizi hilo kwani, makosa
yaliyofanywa hayarekebishiki.
“Haya maombi nayatupilia mbali
hayana miguu ya kusimamia, ni kosa kubwa hati kusainiwa na mtu mwingine
halafu ikathibitishwa na mwingine, hakuna namna ya kurekebisha, lazima
sheria ifuatwe na taratibu zake,” alisema.
Awali, Magambo na
wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga ushindi wa
Bulaya, lakini ilitupiliwa mbali kutokana na kushindwa kutimiza masharti
ya sheria.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka
jana, Bulaya alipata kura 29,973 na Wasira wa CCM aliambulia 19,123
ikiwapo tofauti ya kura 10,000.
Hata hivyo, Wasira alilalamikia matokeo hayo akidai uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu.
Post a Comment