
Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.
Wawili
hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini
habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri
kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Ndoa
hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010
aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado
anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.
Mume
huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie
haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.
Post a Comment