Askofu wa kanisa la Angilikana Dayosisi ya Rift Valley John Lupaa amemshauri Waziri wa elimu Joyce Ndalichako kushughulikia changamoto zinazozikabili shule za msingi Wilayani Manyoni.
Askofu lupaa alitoa
kauli hiyo jana alipotembelea shule ya msingi Sayuni iliyopo manyoni
mjini na kukabidhi jumla ya madawati kumi na saba yenye thamani ya
shilingi laki sita na elfu hamsini.
Akikabidhi madawati hayo Lupaa alisikitishwa kuona wanafunzi wengi wakiwa hawana madawati na kulazimika kukaa chini .
Kufuatia hali hiyo Askofu Lupaa aliiomba serikali kuziangalia kwa jicho
la tatu shule zote za msingi Wilayani hapa ili kuboresha afya na elimu
bora kwa wanafuni.
Katika hatua nyingine Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Stanley Jumamosi amewaomba wadau mbalimbali wa elimu
kujitokeza kuchangia madawati katika shule hiyo ili kuondokana na uhaba
wa madawati.
Mwalimu Jumamosi alisema pamoja
na kwamba wana uhaba wa madawati lakini pia majengo hayatoshelezi
kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi kufuatia tamko la Serikali kutoa
elimu bila malipo.
"Tunaishukuru Serikali
kutambua changamoto ya elimu Tanzania na kuamua kutoa elimu bure lakini
pia inapaswa kufanya utafiti upya kutokana na ongezeko la wanafunzi hali
inayofanya kukosa madawati na vyumba vya madarasa."alisema.
Aidha aalisema ruzuku inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuendeshea
shule haikidhi haja hali inayopelekea kushidwa kulipa baadhi ya garama
za mlinzi maji na umeme.
Pamoja na hayo
Jumamosi aliwapongeza wanafunzi wa shule hiyo kwa ufaulu mzuri licha ya
kukabiliwa na changamoto mbalimbali.
Shule ya
msingi Sayuni imekuwa na muonekano mzuri kielimu ambapo mwaka juzi
ilifanikiwa kuwa ya kwanza kimkoa wakati mwaka jana ikashuka kiwango na
kuwa ya pili ki wailaya hali inayosababishwa na msongamano wa wanafunzi
wengi katika darasa moja.MWISHO
Post a Comment