Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa amewataka waliopewa mamlaka na dhamana mbalimbali Katika jamii kusimamia haki na ukweli hata ikibidi kupoteza maisha kuliko kufuata mashinikizo na kufanya maamuzi yatakayoumiza Wasiokuwa na hatia.
Akihubiri katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa katika
Kanisa Katoliki la Maximilian Kolbe Mwenge Askofu Nzigilwa amesema ni
heri kujiuzulu kazi kuliko kufuata mashinikizo kwa maslahi ya watu
kuvunja haki na amewataka wakristu kuishi maisha ya Sadaka kwa ajili ya
kuinua wengine kama Yesu Kristu alivyokubali kutoa uhai wake kwa ajili
ya ukombozi wa ulimwengu huku akiwaasa kuacha maisha ya visasi kwa kuwa
sio maisha ya kikristu.
Aidha ameusia waumini kuacha tamaa na kuonesha upendo wa kweli kwa
wengine badala ya kuwa wasaliti ili wasiwe sababu ya Kuumizwa kwa
binadamu wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.John Pombe Magufuli na mkewe
amejumuika na mamia ya waumini kwenye ibada ya Ijumaa Kuu Katika Kanisa
la mtakatifu Petro Oysterbay .
Post a Comment