Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC
dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
huku kiingilio cha chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).
Kiingilio
cha juu cha mchezo huo kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa
VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti
vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya
rangi ya bluu na kijani.
Tiketi za
mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika
vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu
(Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa,
Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.(VICTOR)
Mchezo
huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati
Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel
Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa
mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).
Ligi hiyo
ya Vodacom itaendelea Jumamosi kwa michezo sita, Young Africans v Simba
(Taifa), Mbeya City v Azam (Sokoine), Stand United v JKT Ruvu
(Kambarage), Toto Africans v Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting
v Tanzania Prisons (Mkwakwani) na Majimaji FC v Mtibwa Sugar
(Majimaji).
Jumapili
ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC v Coastal Union
uwanja wa Mwadui Complex, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African
Sports uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara.
Post a Comment