Wapiganaji wa Islamic State waliouteka mji wa Sirte nchini Libya wameanza kuweka sheria zao.
Kuingana
na wakaazi waliohojiwa na BBC,wapiganaji hao wapatao 1,500 wameweka
sheria kuhusu mavazi yanayotakiwa kuvaliwa na wanawake au
wanaume,Ubaguzi ndani ya Madarasa ya shule na uanzilishi wa maafisa wa
polisi wa kidini.Mabango ya bara barani yanayowaelekeza wanawake wanavyopaswa kuvaa kwa mujibu wa Sharia yaliwekwa mjini Sirte mwezi Julai 2015.
Picha iliowekwa juu iliandikwa ifuatavyo:
Maelekezo juu ya uvaaji wa hijab kwa mujibu wa Sharia
1. Lazima iwe nzito isiyoonyesha mwili
2. Lazima ilegezwe ( nasio iliyobana)
3. Lazima ifunike mwili wote
4. Haipaswi kuwa ya kuvutia
5. Haipaswi kufanana na nguo za wasioami na wanaume
6.Haipaswi kuwekwa urembo na ya kuvutia macho
Post a Comment