Waliosalia katika kinyang'anyiro cha
kutaka kuwania kupeperusha bendera ya urais kupitia chama cha
Democratic nchini Marekani, Hillary Clinton na Bernie Sanders wanafanya
mdahalo wao wa kwanza wa ana kwa ana kuelekea katika kura ya maoni
itakayofanyika katika Jimbo la New Hampshire.
Sanders amemlaumu
mpinzani wake kwa kuwa kupata mteremko, tuhuma ambazo Bi Clinton
mwenyewe amezibeza na kusema kuwa anajaribu kupata uteuzi wa kuwa
mgombea wa kwanza wa kike.Wanasiasa hao pia wamekwaruzana kuhusu fedha za kampeni na fedha za huduma ya afya na elimu.
Mchuano huo wa Democrat ulipamba moto baada ya Sanders kuunyemelea kwa karibu mno ushindi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje katika mchuano uliofanyika huko jimboni IOWA.
Post a Comment