Wapiganaji 48 walioasi mwito wa
kundi la wapiganaji la Al shabab kutoka Somalia wametunukiwa mtaji na
vifaa vya kutegea uchumi na serikali ya Kenya.
Vijana hao 48 walipewa jokofu na pikipiki ilikuanza upya maisha yao.Katibu katika wizara ya usalama wa ndani wa Kenya Karanja Kibicho aliiambia BBC kuwa vijana hao 48 ndio walioitikia mwito wa serikali kwa wale vijana waliokuwa wamepata mafunzo kutoka kwa kundi hilo la kigaidi kujisalimisha kwa serikali.
''Wale walioitikia mwito huo ndio waliopelekwa kwa mafunzo ya uzalendo na sasa wamehitimu'' alisema bwana Kibicho
Kati ya hao waliohitimu walipewa mtaji wa jokofu na mtaji ilikufanikisha biashara yao ya uvuvi.
Kundi lingine lililopendelea biashara ya uchukuzi walipewa pikipiki zitakazofanikisha biashara ya ''boda boda''.
Vijana wengi waliohojiwa na serikali ya Kenya walilaumu ukosefu wa ajira kama kivutio cha kujiunga na kundi hilo la wapiganaji linalowalipa kuishambulia Kenya
Kundi la Alshabab limekuwa likitekeleza mashambulizi nchini Kenya likisisitiza kuwa nchini hiyo ya Afrika Mashariki sharti iondoe majeshi yake nchini humo.
Kenya ilipeleka majeshi yake nchini Somalia kwa nia ya kuizuia isishambuliwe na magaidi.
Post a Comment