BREAKING NEWS

Monday, 8 February 2016

Mkuu Wa Mkoa Wa Kilimanjaro Amos Makalla Akagua Mpaka Wa Tanzania Na Kenya Na Kuteketeza lita 140 za Gongo



 
Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Kilimanjaro imeteketeza lita 140 za gongo, mapipa 40 na mitambo sita ya kutengeneza pombe hiyo haramu vyenye thamani ya Sh10 milioni.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala, alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Rombo 
Alisema  mitambo hiyo  ya  gongo  iliteketezwa  katika  kijiji  cha Kikelelwa  Tarakea  wilayani  humo.
Makala  alisema  pombe  hiyo  imekuwa  ikileta  madhara  kwa  wananchi  hasa  vijana  ambao  wamekuwa  wakishindwa  kufanya  shughuli  za  maendeleo  kutokana  na  kunywa  muda  wa  kazi
 Alisema  wilaya  hiyo  inaongoza  kwa  kutengeneza  pombe  za  kenyeji  zaidi  ya 50  kwa  kutumia  kemikali  hatarishi.
  
"Gongo inaathari kubwa kutokana na utengenezaji wake, nimeambiwa wanaweka maji ya betri na kinyesi cha binadamu,” alisema Makala.

Alisema pombe hiyo inatajwa kuharibu nguvu za kiume na kupoteza nguvu kazi kubwa kwa Taifa hali inayosababisha kazi za wanaume kufanywa na wanawake.

Awali, kamati hiyo ya ulinzi na usalama ilikagua mipaka ya Kenya na Tanzania kuanzia Holili hadi Tarakea.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo, alisema anapambana kukomesha unywaji wa pombe saa za kazi na utengenezaji wa pombe hizo.

Alisema wataendelea kukamata mitambo pamoja  na  malighafi  za  kutengeneza  pombe hizo
 
 
 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wakikagua mpaka wa Tanzania na Kenya 

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree